BeroGenge
🏢 Address: OPPOSITE na chuo cha ustawi wa jamii, barabara ya sinza, bamaga, DAR ES salaam Tanzania
About This Business
TununuePamoja ni mfumo ambao tunakuwezesha kuagiza bidhaa kutoka China kwa kushirikiana na wengine ili kuweza kufikia kiwango cha Chini (MOQ) kinachopangwa na viwanda au wachuuzi wakubwa, LENGO upate bidhaa kwa bei nafuu. pia Tuagize chochote China.
TununuePamoja ni nini?@berogenge
TununuePamoja ni moja kati ya huduma zetu, na kupitia mfumo huu tunakuwezesha kuagiza bidhaa kutoka China kwa kushirikiana na wengine ili kuweza kufikia kiwango cha Chini (MOQ) kinachopangwa na viwanda au wachuuzi wakubwa na kujipatia bidhaa kwa bei nafuu.
Huduma huu tunaitoa kupitia magroup yetu ya whatsapp na pia kwa mtandao wetu ambao unakua kwa kasi sana nchini Tanzania www.tununuepamoja.com.
Tunafanya nini hasa?
TununuePamoja.com kwa umakini na umahiri tunahakikisha upatikanaji wa bidhaa zilizo bora kutoka China, tunapokea oda zako, tunakusafirishia mzigo hadi kwenye stoo zetu na pia tunahakikisha kila mmoja anapata mzigo wake kulingana na idadi aliyoagiza. Mfumo huu ni rahisi kutumia na ni rafiki kwa mtumiaji.
1⃣Tunapatikana wapi?
Stoo zetu zipo Dar es Salaam karibu stendi ya zamani ya Bamaga barabara ya sinza tunatazamana na chuo cha utumishi.
2⃣Tunasafirishaje mizigo?
Kwa kawaida mizigo tunasafirisha kwa njia ya ndege na meli na tunajitahidi katika kuchagua kampuni ambazo zinasafirisha mizigo kwa uharaka na uhakika.
3⃣Mizigo inachukua siku ngapi kufika stoo yetu?
Inachukua siku 7 hadi 12 kwa usafiri wa ndege.
Inachukua siku 35 hadi 60 kwa usafiri wa maji. 
4⃣Vipi kuhusu watu wa mikoani?
Tayari BeroGenge tumeanza kujitanua kuwafikia watu wa mikoa mingine, na baadhi ya mikoa tayari tuna mawakala na tunaendelea kutafuta mawakala zaidi kufikia mikoa yote ya Tanzania. Utaratibu wa sasa, baada ya mizigo kufika stoo yetu utatumiwa kama upo mkoa mwingine.
5⃣Jinsi ya kuweka Oda
Kuweka oda ni rahisi na salama, tembelea www.tununuepamoja.com maelekezo ni rahisi au wasiliana nasi.
Agiza bidhaa kutoka China kwa kutumia mtandao wako wa kijanja www.tununuepamoja.com kwa bidhaa zenye ubora na uhakika.
#TununuePamoja 
#berogenge
Contact Information
No Products Listed Yet
This business hasn't added any products to their catalog yet.